TOP 5 BEST BONGO RAPPER OF ALL TIME

TOP 5 BEST  BONGO RAPPER OF ALL TIME


Okey, ni kwa muda sana nimekuwa nikitaka kuandika kuhusu swala hili ya rapper bora wa siku zote kwetu hapa Tanzania, Lakini nimekuwa sipati muda kutokana na harakati na projects tofauti tofauti za kimaisha. Lakini kwa neema ya Mungu leo nimepata muda na nikaona sio vibaya nikaandika kuhusu swala hili, 

Kabla ya kuandika swala hii napenda kutoa vigezo nilivyotumia kuweza kutengeneza list hii ya rappers watano wakali wa siku zote kutoka hapa kwetu Tanzania ni kama ifuatavyo

  1. Uwezo wa uandishi wa mashairi
  2. Uwezo wa kufikisha Ujumbe kwa hadhira 
  3. Uwezo wa kuhimili maada husika katika nyimbo husika
  4. Uwezo binafsi 
  5. Idadi ya nyimbo bora kutoka kwa msanii husika
Bila kupoteza muda naomba tuanze pamoja kuhesabu list yetu ya Top 5 best bongo rapper of all time 

5. Nikk Mbishi 



Namba tano anasimama Nikk Mbishi a.k.a Dr Unju bin uniq, Yeah najua watu wengi wata jiuliza kwanini nikk na sio rapper fulani. . Na shidwa kujiuliza why Mbishi hujiita Unju wasipate jibu lolote okey sio tabu unaweza soma nakala hii Hapa unaweza pata kitu na kutoa utata huo na kuelewa kiundani uwezo wa NICAS 

Watu wengi wanaweza niuliza why ?, Nikk Mbishi. Jibu ni dogo tu "UWEZO" Nikk ni moja kati ya rapper wenye confidence na kuamini binafsi ni moja kati ya rapper bora, Nikk ni kati ya rapper asiwe pelekeshawa na media wala mtu binafsi, Nikk ni  moja kati ya rapper wenye uwezp wa ku stick kwenye maada hasa pale anapo chana, Moja kati ya nyimbo amabazo nikk alisha wahi fanya na kuwa bora kuwahi tokea ni pamoja na KIJUSI, AU, HISIA, KILA SIKU kama umaweza pata hizo nyimbo na kuzisikiliza japo mara tatu kila siku unaweza kubaliana na mimi 

Pia kitu kilichofanya nikk kuwa katika list hii ni uwezo wake wa kuto choka kutoa ngoma, Washikaji wengi wamekuwa wakisema nikk ni kisima cha mziki hakiwezi kau leo wala kesho, kila siku nikk harakati mwanzo mwisho 

4. Jcb  Makalla 




Ukisikia Paaa!! Ujue imekukosa... Jcb makalla moja kati ya rapper wakali tokea Arusha japo kwa sasa kifamilia yupo aboard. Watu wengi wana weza shangazwa na list hii but kwa wafatiliaji  wa muda mrefu hawawezi bishana na mimi uwezo wa JCB ni mkubwa sana hasa kiuandishi na ku-rap JCB ni moja kati ya rapper pale unapo wapa topic ya kuzungumzia hufanya kitu roho inapenda

JCB ni moja kati ya rapper wenye flow adimu sana kwenye mziki wa bongo tofauti na rapper wa kisasa kila rapper akiflow ni yale yale tu, But hata ukiwa usingizini JCB ni kati ya rapper atakufanya uamke ukiwa usingizini, ukae na usikilize kwa makini na naamini mwisho ya nyimbo lazima upate kitu na utikise kichwa 

Namba nne yetu kwa leo imekwenda kwa JCB rapper mkongwe ma makini toka Arusha 



3. Jay Moo



Jay moo, mzee wa stori tatu tofauti, hit maker wa pesa madafu. Jay moo ni moja ya wasanii wa zamani kwenye mziki wa bongo hip hop, Kutokana na uwezo wake chini ya usimamizi wa producer bora bongo a.k.a father of bongo fleva P-Fank Majani  amekuwa msanii ambaye hutoma nyimbo zale kwa muda na kufanya vizuri

Jay moo ni moja katika ya rapper wanaopatika katika kundi la WATEULE akimemo SOLO THANG, MCHIZ MOX. Sababu kubwa iliyonifanya kuweza kumuweka Jay moo  kwenye hii list ni pamoja na idadi ya hit song zake ambazo alisha kwisha zitoa toka muda mrefu na kuwa bora zilizo andikwa katika ujuzi wa hali ya juu ndani ya msingi ya hip hop na ujumbe katika nyimbo zake zote


2. Fid Q






Fid Q a.k.a Jeshi la mtu mmoja, rapper toka mwanza rapper mwenye uandishi mgumu kuelewa na utunzi wa hali ya juu. Kitu kinacho mtofautisha Fid Q na rapper wengi bongo ni uwezo wa kutumia kiswahili na misamiati migumu kwenye mziki wake, 

Kila mtu anajua uwezo wake katika rapping career, ni moja katika ya rapper wanaoshikilia tuzo ya best male hip hop artist. Fid ni moja kati ya rapper wenye hit song nyingi sana na zenye ujumbe mkali. Wengine humuita fid kuwa ni Nas wa bongo kutokana na uwezo wake wa uandishi na story katika nyimbo zake 


1. Profesa Jay






Mwana msolopa ganzi, wa mitulinga father of bongo rapping career, Pro Jay ni moja kati ya rapper waliofanya mziki huu wa bongo hip hop kufika hapa ulipo kutokana na uwezo wake Pro Jay ameweza ku washawishi wazazi wa rapper wengi wa sasa kuweza kufungua milango kwa watu wengi kuamini kuwa mziki sio uhuni

Pro Jay kwa sasa ni mbunge katika maswala ya kiserikali ni moja kati ya wasanii wenye uwezo mkali wa utunzi wa nyimbo zenye ujumbe mkali na zenye maadili katika jamii

Pro Jay ni rapper walio kaa katika game hili la hip hop kwa muda mrefu sana bila kupotea wa kuteteseka ndio sababu kubwa ililo fanya kuwa katika list hii hasa namba moja pia  






1 maoni:

UMEMKOSEA HESHIMA FID Q KUMUITA BEST FEMALE RAPPER

Reply

Chapisha Maoni