FID Q KUVUKA MIPAKA MPAKA NIGERIA KWA MKALI 2 FACE.



Ni fulaha kubwa sana kwangu kuona mziki wa hip hop Tanzania ukikua kila siku kutoka step moja kwenda step nyingine hivyo inatupa faraja hasa sisi wa dau wa huu mziki wa hip hop kuto kukata tamaa na kuamini ipo siku tutafika tunapo taka kwenda.
Swala la fulaha kimetokea baada ya mkali wa hip hop tanzania fid q kutoa tetesi katika chombo fulani cha redio kuwa mashabiki wake wakae mkao wa kula any time anaweza fanya kazi na mkali wa miondoko ya RnB 2FACE kutoka Nigeria kwani wamesha wahi kukutana nakupanga mipango hiyo since long time sema harakati zikawa zinawabana  but kwa neema za Mungu zaidi ni pale majuzi juzi  rapper fidq alipo kutana na msanii huyo alipo kuwa katika harakati za coke studio na kupanga mipango endelevu ya pale walipo ishia 
Sisi kama wa dau wa mziki tuna waombea uzima ili watupe mziki mzuri kama tunavyo talajia.

TOKA KWA ONE INCREDIBLE : NEW MIXTAPE "IDENTITY" COMING SOON.



Rapper One the Incredible ambaye ni moja Kati ya rapper wanao unda kundi la tamaduni muzik ameliweka swala hilo wazi katika ukurasa wake wa INSTAGRAM akiwataarifu wapenzi wake wa kanda mseto (mixtape) wakae mkao wakula kwani mixtape yake kali inayo kuja ambayo ipo katika hatua za mwisho wisho kabisa katika maandalizi ya kutoka.

Ni imani yangu hii itakuwa ni mixtape kali wahi tokea kwa mwaka huu wa 2015 kwani kila mtu anajua uwezo wa rapper one linapokuja swala la kunata na midundo na umahili wa uandishi..
Pia rapper One incredible amesema kwamba mixtape yake ataitoa bure kabisa bila malipo yoyote kitu ambacho ni moja kati ya vitu vilivyo fanya watu wengi waweze kutoamini swala hilo kwani itakuwa ni mala ya kwanza kutokea katika music industry ya bongo. But all in All tukae tayari kwa ajira ya "IDENTITY"

NI TIME YA RAPPER MABESTE: NDOA




Rapper mabeste yuko mbioni muda wowote kufunga ndoa na mpenzi wake mpendwa walio pendana kwa muda mrefu katika kipindi cha laha na matatizo. Rapper mabeste amelionesha hilo wazi kwa wapenzi wake kuwa anampenda sana mpenzi wake kwani hata mwanzo kipindi ana pata matatizo mabeste alikuwa bega kwa bega na mpenzi wake .Pia alipo pata tatizo kubwa  hakuona hatari kuomba msaada kwa fans wake hata wasanii wenzake. Mabeste ni rapper amabaye amefanikiwa kupata mtoto mmoja mpaka sasa.

Mabeste amefika uamzi huo baaada ya kuona  now ni muda wa yeye kuvuta jiko japo ametahadhalisha kuwa swala hilo linaweza kuwa la kushitukiza, kwahiyo watu wawe tayari kwa lolote iwe kimchngo au any support.

NEW TRACK COMING SOON P THE NATIVE ft JORDAN- CHINI YA JUA.



Kama hujawahi pata nafasi na kumsikiliza vizuri P the Native utakuwa unakosa kitu ili kukamilisha chat yako ya  underground rapper wakali katika music industry ya Tanzania. Naamini ukipata muda ukatulia na kisikia japo ngoma moja yake aliyo toa,napendekeza utafute ngoma yake inayo kwenda kwa jina la UWEZO amemshirikisha Mulla asee ni moja ya ngoma kali sana kusema  ukweli.Kinachonifulahisha kumsikiliza p tha native ni uwezo wa kutumia street language au kwa kiswahili tunaiita "lugha ya mtaa" kufikisha ujumbe kwa hadhila. Katika swala la uandishi wa beti zake itakuchukua muda kidogo kuweza kumuelewa kwani ni moja ya rapper wasio tumia mtiriliko wa uandishi uliozoeleka kitu kinacho fanya rapper wengi kutumia aina hii ya uandishi linapokuja swala la DISS.

New Joint inayokuja toka kwa P the native ni Ngoma inayokwenda kwa jina la "CHINI YA JUA" naamini ni bonge la ngoma maana always rapper bora ni bora siku zote hata kama asipotoa ngoma mpya.Mitaa ikae mkao wa kula kupokea mziki mzuri.

FID Q AINGIZWA KWENYE ORODHA YA WASANII 20 BORA WA HIP HOP AFRICA



Fid Q ni moja wa rapper bora sana walio wahi tokea katika ramani ya mziki wa hip hop hapa kwetu Tanzania,Kama kweli wewe ni mfatiliaji mzuri wa mziki wa hip hop huwezi kubishana na mimi, Kwani mpaka sasa naweza sema ni mfalme wa Hip hop Tanzania,kinacho mtofautisha Fid Q na rappers/wachanaji wengine hapa nchini ni uwezo wake wa  ki uandishi wa mashairi,linapo kuja swala la kuandika mashairi siku zote Fid Q huwa hakosei katika kuandika mashairi makali na magumu kudadavua na  pia  hutumia pia ufundi wake aliopewa na mwenyezi mungu wa kutumia lugha ya kiswahili vizuri na kuhakikisha  masharii yake yanakuwa katika kiwango chake cha juu.

Kutokana na hayo basi jalida la SA HIP-HOP limempa nafasi nyingine Fid Q kutambulika Kia afrika kwa kuweza kuamini uwezo wake wa uandishia wa Mashairi na kumuingiza katika orodha ya Majina  20 ya wasanii bora Afrika na fid Q akikamata nafasi ya 18 akiwa Mtazania pekee kupata nafasi hiyo. wasanii wengine walio unda Orodha hiyo ni kama ifuatavyo.



1. AKA - South Africa.

2.Sarkordie - Ghana.

3.Ice prince - Nigeria

4.Cassper Nyovest - South Africa

5.M.I - Nigeria.

6.KO - South Africa

7.Manifest - Ghana

8.k'naan - Somalia

9. Zues - Botswana

10. Phyon - Nigeria.

11. Olamide -  Nigeria

12. Dee Money - Ghana

13. Octopizzo - Kenya

14. Tumi - South Africa

15. Stunner - Zimbambwe

16. Yossoupha - Congo

17. Dama Da Bling - Msumbiji

18. Fid Q - Tanzania

19. Cleo ice Queen - Zambia

20. Cal Vin - Zimbambwe



Hapo ndipo Fid Q aliweza kuwa katika list hiyo na kuwa rapper bora na pekee kwa Tanzania kutokea katika jalida hilo la SA HIP-HOP.