NEW MIX-TAPE FROM WAKAZI COMING SOON



Webiro N Wakazi maarufu kama WAKAZI yupo mbioni kuachia mixtape (Kanda Mseto) yake mpya hivi karibuni
, ni kwa muda mrefu WAKAZI amekuwa akisikika kuwa yupo katika harakati za kuandaa mixtape yake mpya ambayo mpaka sasa haijafahamika itakwenda kwa jina gani, But ni matalajio yangu kuwa itakuwa moja kati ya mix-tape  nzuri maana sina wasiwasi na uwezo wa WAKAZI hasa katika uandaaji wa mixtape kali maana ana uzoefu mkubwa katika uandaji wa album nzuri na kanda mseto na sio mala yake ya kwanza kufanya jambo hii katika ufanisi mkubwa!

Wakazi mpaka sasa ajatamka siku rasimi ambayo ataachia kanda mseto yake  hiyo mpya kwa sababu anasema kuwa kuna baadhi ya mambo bado anayaweka sana na kama yakikaa sawa kama anavyotaka atakuwa hana kipingamizi tena cha kumfanya asiachie kanda mseto hiyo inayo subiliwa kwa shauku kubwa mtaani

Pia kuna uwezekano kuwa wakazi akawa katika mpango pia wa kuachia album yake mpya baada ya kuachia mixtape yake mpya inayo subiliwa na watu wengi mtaani na mimi nikiwa mmoja kati yao. Kama alivyo tamka katika mahojiano ya kipindi cha Ladha3600  kinacho lushwa na redio ya E-fm chini ya utangazaji wa Jabir Saleh , namnukuu;
Nitaachia Mixtape siku za karibuni kabla ya Album kwasababu kuna vitu bado havijakaa sawa
 Hivyo mpaka sasa hatujajua tarehe na siku rasimi ambayo wakazi atatoa mixtape yake ikifatiwa na album yake mpya. Lakini kaa tayari kwa ujio wa kishindo kutoka kwa wakazi. Kinachotakuwa kwako kama shabiki wa kweli ni support yako ya nguvu ili kuweza kufikisha mziki huu wa bongo hip hop mbali zaidi ya hapa ulipo . Pia taarifa hizo utaendelea kuzipata hapa bure kwenye tovuti hii yetu pendwa.

NEW AUDIO: NIKKI MBISHI FT HARD MAN - GOOD VIBES



Download good new music kutoka kwa nikk mbishi ft hard man GOOD VIBES, round hii kwenye nyimbo yake mpya nikki amefanya kitu cha maana na ziada kwa kumshirikisha msanii wa zamani sana na aliye kuwa silent sana kwenye industry ya mziki bila mashabiki zake kujua kipi kilimpata kwa muda wote huu kuwa silent.

Ki-ufupi nyimbo ni nzuri na ina miondoko ya hip hop unaweza pata nakala yako HAPA na kusikiliza na pia kutoa maoni yako kuhusu nyimbo hii, Pia unaweza share na rafiki zako na jamaa ili kuweza kutoa support kwa namna moja au nyingine katika kukuza mziki wa BONGO HIP HOP asante!. 

NEW AUDIO: GOOD MUSIC - BINGO (Boy Stimela) ft EDDY MC

 New bongo hip hop music toka kwa bingo a.k.a Boy Stimela


New bongo hip hop music toka kwa bingo a.k.a Boy Stimela ft Eddy Mc, Moja katika ya wasanii tokea Dar wenye uwezo mzuri wa kuandika na kuflow vizuri haswa linapokuja swala la mziki mzuri katika lugha ya kiswahili. Pia ni moja kati ya rapper walio kwisha fanya mziki toka zamani na rapper maarufu kama STEREO na wengine toka Dar.

Unaweza pata nakala ya nyimbo hiyo HAPA na kuisikiliza kwa umakini na unaweza kunambia kipi umekiona kwa rapper huyu je ?, Anaweza au laa!!

Nyimbo imefanyika chini ya studio ya 99 Records.

NEW VIDEO: MNAZ MC ft CHINDO MAN - I'M PEACE




Mnaz Mc ni moja kati ya wasanii wapya kwenye mziki wa bongo hip hop tokea ARUSHA, Pia nikati ya wasanii waliopo chini ya record label ya WATENGWA RECORD chini ya usimamizi wa chindo man rapper bora na mahiri tokea ARUSHA japo kimaisha mara nyingi yupo abroad

Watu wengi watakuwa hawamfahamu rapper huyu  kutokana na kuwa mgeni masikioni mwa wasikilizaji wa mziki wa bongo HIP HOP wengi, But wait ni kwambie kitu..!!

Je wajua Mnaz MC was winner of African Music Now Freestyle Battle in Kijenge Juu, moja ya sifa inayoweza kukupa ushawishi wakumsikiliza kwa umakini na kumpokea katika mziki wa BONGO HIP HOP ili aweze kukimbiza kijiti kama rapper wengine wakwogwe au wapya katika mziki huu wa bongo hip hop

VIDEO imefanyika chini ya usimamizi wa Africanmusicnow na kuwa filmed and directed by Dony and Davy K of D.I.D. Entertainment. Waweza itazama video hiyo hapa chini na kutoa support yako kwa kushare na watu mbali mbali ili kuweza kufikisha mziki wetu wa bongo hip hop mbali..



NEW AUDIO: SISI - GODZILLA ft STEREO ft ONE THE INCREDIBLE ft NIKK MBISHI

 Godzilla ft One the Incredible ft Stereo ft Nikk Mbishi inayokwenda kwa jina la SISI


Download nyimbo mpya kutoka kwa Godzilla ft One the Incredible ft Stereo ft Nikk Mbishi inayokwenda kwa jina la SISI,  Kama kawaida ujuavyo katika mziki wa HIP HOP  wanapokutana wa kali katika bongo hiphop music huwa kila mtu kwa uwezo wake binafsi kujitahidi kufanya kitu kizuri kwa ajili ya mashabiki wake wake na hapo ndipo mziki mzuri hutokea.

Kila mtua anajua uwezo wa wa saniii hawa ki-uwezo binafsi mmoja baada ya mmoja kwa hiyo kazi kwako kusikiliza nyimbo ki-umanikini na kutuoa mtanzamo wako kipi umependa katika nyimbo zima na kipi hujakiependa

Nyimbo hii umetayarishwa na producerKIBABU WAPOTEEN  chini ya studio ya KILI RECORDS 

Nyimbo unaweza kuipakua HAPA pia na  kushare na wapenda mziki wa hip hop na kutoa support yako katika mziki wa bongo hip hop kwa namna moja au nyingine.