NEW MIX-TAPE FROM WAKAZI COMING SOON



Webiro N Wakazi maarufu kama WAKAZI yupo mbioni kuachia mixtape (Kanda Mseto) yake mpya hivi karibuni
, ni kwa muda mrefu WAKAZI amekuwa akisikika kuwa yupo katika harakati za kuandaa mixtape yake mpya ambayo mpaka sasa haijafahamika itakwenda kwa jina gani, But ni matalajio yangu kuwa itakuwa moja kati ya mix-tape  nzuri maana sina wasiwasi na uwezo wa WAKAZI hasa katika uandaaji wa mixtape kali maana ana uzoefu mkubwa katika uandaji wa album nzuri na kanda mseto na sio mala yake ya kwanza kufanya jambo hii katika ufanisi mkubwa!

Wakazi mpaka sasa ajatamka siku rasimi ambayo ataachia kanda mseto yake  hiyo mpya kwa sababu anasema kuwa kuna baadhi ya mambo bado anayaweka sana na kama yakikaa sawa kama anavyotaka atakuwa hana kipingamizi tena cha kumfanya asiachie kanda mseto hiyo inayo subiliwa kwa shauku kubwa mtaani

Pia kuna uwezekano kuwa wakazi akawa katika mpango pia wa kuachia album yake mpya baada ya kuachia mixtape yake mpya inayo subiliwa na watu wengi mtaani na mimi nikiwa mmoja kati yao. Kama alivyo tamka katika mahojiano ya kipindi cha Ladha3600  kinacho lushwa na redio ya E-fm chini ya utangazaji wa Jabir Saleh , namnukuu;
Nitaachia Mixtape siku za karibuni kabla ya Album kwasababu kuna vitu bado havijakaa sawa
 Hivyo mpaka sasa hatujajua tarehe na siku rasimi ambayo wakazi atatoa mixtape yake ikifatiwa na album yake mpya. Lakini kaa tayari kwa ujio wa kishindo kutoka kwa wakazi. Kinachotakuwa kwako kama shabiki wa kweli ni support yako ya nguvu ili kuweza kufikisha mziki huu wa bongo hip hop mbali zaidi ya hapa ulipo . Pia taarifa hizo utaendelea kuzipata hapa bure kwenye tovuti hii yetu pendwa.

NEW AUDIO: NIKKI MBISHI FT HARD MAN - GOOD VIBES



Download good new music kutoka kwa nikk mbishi ft hard man GOOD VIBES, round hii kwenye nyimbo yake mpya nikki amefanya kitu cha maana na ziada kwa kumshirikisha msanii wa zamani sana na aliye kuwa silent sana kwenye industry ya mziki bila mashabiki zake kujua kipi kilimpata kwa muda wote huu kuwa silent.

Ki-ufupi nyimbo ni nzuri na ina miondoko ya hip hop unaweza pata nakala yako HAPA na kusikiliza na pia kutoa maoni yako kuhusu nyimbo hii, Pia unaweza share na rafiki zako na jamaa ili kuweza kutoa support kwa namna moja au nyingine katika kukuza mziki wa BONGO HIP HOP asante!. 

NEW AUDIO: GOOD MUSIC - BINGO (Boy Stimela) ft EDDY MC

 New bongo hip hop music toka kwa bingo a.k.a Boy Stimela


New bongo hip hop music toka kwa bingo a.k.a Boy Stimela ft Eddy Mc, Moja katika ya wasanii tokea Dar wenye uwezo mzuri wa kuandika na kuflow vizuri haswa linapokuja swala la mziki mzuri katika lugha ya kiswahili. Pia ni moja kati ya rapper walio kwisha fanya mziki toka zamani na rapper maarufu kama STEREO na wengine toka Dar.

Unaweza pata nakala ya nyimbo hiyo HAPA na kuisikiliza kwa umakini na unaweza kunambia kipi umekiona kwa rapper huyu je ?, Anaweza au laa!!

Nyimbo imefanyika chini ya studio ya 99 Records.

NEW VIDEO: MNAZ MC ft CHINDO MAN - I'M PEACE




Mnaz Mc ni moja kati ya wasanii wapya kwenye mziki wa bongo hip hop tokea ARUSHA, Pia nikati ya wasanii waliopo chini ya record label ya WATENGWA RECORD chini ya usimamizi wa chindo man rapper bora na mahiri tokea ARUSHA japo kimaisha mara nyingi yupo abroad

Watu wengi watakuwa hawamfahamu rapper huyu  kutokana na kuwa mgeni masikioni mwa wasikilizaji wa mziki wa bongo HIP HOP wengi, But wait ni kwambie kitu..!!

Je wajua Mnaz MC was winner of African Music Now Freestyle Battle in Kijenge Juu, moja ya sifa inayoweza kukupa ushawishi wakumsikiliza kwa umakini na kumpokea katika mziki wa BONGO HIP HOP ili aweze kukimbiza kijiti kama rapper wengine wakwogwe au wapya katika mziki huu wa bongo hip hop

VIDEO imefanyika chini ya usimamizi wa Africanmusicnow na kuwa filmed and directed by Dony and Davy K of D.I.D. Entertainment. Waweza itazama video hiyo hapa chini na kutoa support yako kwa kushare na watu mbali mbali ili kuweza kufikisha mziki wetu wa bongo hip hop mbali..



NEW AUDIO: SISI - GODZILLA ft STEREO ft ONE THE INCREDIBLE ft NIKK MBISHI

 Godzilla ft One the Incredible ft Stereo ft Nikk Mbishi inayokwenda kwa jina la SISI


Download nyimbo mpya kutoka kwa Godzilla ft One the Incredible ft Stereo ft Nikk Mbishi inayokwenda kwa jina la SISI,  Kama kawaida ujuavyo katika mziki wa HIP HOP  wanapokutana wa kali katika bongo hiphop music huwa kila mtu kwa uwezo wake binafsi kujitahidi kufanya kitu kizuri kwa ajili ya mashabiki wake wake na hapo ndipo mziki mzuri hutokea.

Kila mtua anajua uwezo wa wa saniii hawa ki-uwezo binafsi mmoja baada ya mmoja kwa hiyo kazi kwako kusikiliza nyimbo ki-umanikini na kutuoa mtanzamo wako kipi umependa katika nyimbo zima na kipi hujakiependa

Nyimbo hii umetayarishwa na producerKIBABU WAPOTEEN  chini ya studio ya KILI RECORDS 

Nyimbo unaweza kuipakua HAPA pia na  kushare na wapenda mziki wa hip hop na kutoa support yako katika mziki wa bongo hip hop kwa namna moja au nyingine.


TOP 5 BEST BONGO RAPPER OF ALL TIME

TOP 5 BEST  BONGO RAPPER OF ALL TIME


Okey, ni kwa muda sana nimekuwa nikitaka kuandika kuhusu swala hili ya rapper bora wa siku zote kwetu hapa Tanzania, Lakini nimekuwa sipati muda kutokana na harakati na projects tofauti tofauti za kimaisha. Lakini kwa neema ya Mungu leo nimepata muda na nikaona sio vibaya nikaandika kuhusu swala hili, 

Kabla ya kuandika swala hii napenda kutoa vigezo nilivyotumia kuweza kutengeneza list hii ya rappers watano wakali wa siku zote kutoka hapa kwetu Tanzania ni kama ifuatavyo

  1. Uwezo wa uandishi wa mashairi
  2. Uwezo wa kufikisha Ujumbe kwa hadhira 
  3. Uwezo wa kuhimili maada husika katika nyimbo husika
  4. Uwezo binafsi 
  5. Idadi ya nyimbo bora kutoka kwa msanii husika
Bila kupoteza muda naomba tuanze pamoja kuhesabu list yetu ya Top 5 best bongo rapper of all time 

5. Nikk Mbishi 



Namba tano anasimama Nikk Mbishi a.k.a Dr Unju bin uniq, Yeah najua watu wengi wata jiuliza kwanini nikk na sio rapper fulani. . Na shidwa kujiuliza why Mbishi hujiita Unju wasipate jibu lolote okey sio tabu unaweza soma nakala hii Hapa unaweza pata kitu na kutoa utata huo na kuelewa kiundani uwezo wa NICAS 

Watu wengi wanaweza niuliza why ?, Nikk Mbishi. Jibu ni dogo tu "UWEZO" Nikk ni moja kati ya rapper wenye confidence na kuamini binafsi ni moja kati ya rapper bora, Nikk ni kati ya rapper asiwe pelekeshawa na media wala mtu binafsi, Nikk ni  moja kati ya rapper wenye uwezp wa ku stick kwenye maada hasa pale anapo chana, Moja kati ya nyimbo amabazo nikk alisha wahi fanya na kuwa bora kuwahi tokea ni pamoja na KIJUSI, AU, HISIA, KILA SIKU kama umaweza pata hizo nyimbo na kuzisikiliza japo mara tatu kila siku unaweza kubaliana na mimi 

Pia kitu kilichofanya nikk kuwa katika list hii ni uwezo wake wa kuto choka kutoa ngoma, Washikaji wengi wamekuwa wakisema nikk ni kisima cha mziki hakiwezi kau leo wala kesho, kila siku nikk harakati mwanzo mwisho 

4. Jcb  Makalla 




Ukisikia Paaa!! Ujue imekukosa... Jcb makalla moja kati ya rapper wakali tokea Arusha japo kwa sasa kifamilia yupo aboard. Watu wengi wana weza shangazwa na list hii but kwa wafatiliaji  wa muda mrefu hawawezi bishana na mimi uwezo wa JCB ni mkubwa sana hasa kiuandishi na ku-rap JCB ni moja kati ya rapper pale unapo wapa topic ya kuzungumzia hufanya kitu roho inapenda

JCB ni moja kati ya rapper wenye flow adimu sana kwenye mziki wa bongo tofauti na rapper wa kisasa kila rapper akiflow ni yale yale tu, But hata ukiwa usingizini JCB ni kati ya rapper atakufanya uamke ukiwa usingizini, ukae na usikilize kwa makini na naamini mwisho ya nyimbo lazima upate kitu na utikise kichwa 

Namba nne yetu kwa leo imekwenda kwa JCB rapper mkongwe ma makini toka Arusha 



3. Jay Moo



Jay moo, mzee wa stori tatu tofauti, hit maker wa pesa madafu. Jay moo ni moja ya wasanii wa zamani kwenye mziki wa bongo hip hop, Kutokana na uwezo wake chini ya usimamizi wa producer bora bongo a.k.a father of bongo fleva P-Fank Majani  amekuwa msanii ambaye hutoma nyimbo zale kwa muda na kufanya vizuri

Jay moo ni moja katika ya rapper wanaopatika katika kundi la WATEULE akimemo SOLO THANG, MCHIZ MOX. Sababu kubwa iliyonifanya kuweza kumuweka Jay moo  kwenye hii list ni pamoja na idadi ya hit song zake ambazo alisha kwisha zitoa toka muda mrefu na kuwa bora zilizo andikwa katika ujuzi wa hali ya juu ndani ya msingi ya hip hop na ujumbe katika nyimbo zake zote


2. Fid Q






Fid Q a.k.a Jeshi la mtu mmoja, rapper toka mwanza rapper mwenye uandishi mgumu kuelewa na utunzi wa hali ya juu. Kitu kinacho mtofautisha Fid Q na rapper wengi bongo ni uwezo wa kutumia kiswahili na misamiati migumu kwenye mziki wake, 

Kila mtu anajua uwezo wake katika rapping career, ni moja katika ya rapper wanaoshikilia tuzo ya best male hip hop artist. Fid ni moja kati ya rapper wenye hit song nyingi sana na zenye ujumbe mkali. Wengine humuita fid kuwa ni Nas wa bongo kutokana na uwezo wake wa uandishi na story katika nyimbo zake 


1. Profesa Jay






Mwana msolopa ganzi, wa mitulinga father of bongo rapping career, Pro Jay ni moja kati ya rapper waliofanya mziki huu wa bongo hip hop kufika hapa ulipo kutokana na uwezo wake Pro Jay ameweza ku washawishi wazazi wa rapper wengi wa sasa kuweza kufungua milango kwa watu wengi kuamini kuwa mziki sio uhuni

Pro Jay kwa sasa ni mbunge katika maswala ya kiserikali ni moja kati ya wasanii wenye uwezo mkali wa utunzi wa nyimbo zenye ujumbe mkali na zenye maadili katika jamii

Pro Jay ni rapper walio kaa katika game hili la hip hop kwa muda mrefu sana bila kupotea wa kuteteseka ndio sababu kubwa ililo fanya kuwa katika list hii hasa namba moja pia  






SONGA - YULE JAMAA - NEW VIDEO



Moja kati ya rapper ninao ejoy kuwasikiliza kila muda bila kuchoka ni pamoja na SONGA, Songa ni moja kati ya  rapper wanaotambulika  E. Africa kwa  kutumia kiswahili vizuri sana linapokuja swala la uandishi wa mashairi ya kiswali kuweza kuwakilisha ujumbe kwa hadhira.

Songa kwa muda mfupi alikuwa yupo kinywa kidogo, Jambo hilo ilifanya watu wengi pamoja mna mashabiki wake kuwa na hamu na ujio wake katika mziki wa hip hop na kama ilivyo kawaida huwa hakosii kaja na track plus video  moja kali sana kiasi kwamaba ameweza kukidhi ile shauku ya mashabiki wake toka muda mrefu

Safi sana songa huu ujio unaweza kukufanya ukawa msanii tofauti mwenye malengo mpya 2016 unaweza kuitazama video hiyo hapa na kutoa mchango wako kuhusu video hii



ONE OF THE BEST FREESTLY OF ALL TIME FROM - NIKK MBISHI



Nikk Mbishi ni moja kati ya rapper bora wenye uwezo mkubwa sana linapokuja swala ya Freestyle a.k.a (Mitindo Huru) kwa hapa nchini, Nimekuwa nikifatilia kwa karibu sana swala la mitindo huru hapa nchini, lakini wengi wao linapo kuja swala la ku freestlye wengi wao  hukimbilia kuimba  na kupotenza ladha ya mitindo huru.

   Nikk Mbishi ni kati ya rapper ambao hawatoki ndani ya dhana hii ya mitindo huru na siku zote hufanya vyema kuliko wengi wao na hili ndio swala linalo mfanya nikk mbishi  kuingia katika list ya best mc wenye uwezo mkubwa  wa ku-freestyle  maada tofauti tofauti kwa muda mrefu akifatiwa na rapper godzilla kutoke SALASALA

But miaka nenda ludi nikk mbishi hajawahi fanya freestlye kali na yenye mvuto kuliko hii HAPA kinacho nifanya kuipenda freestly hii mitindo huru ya nikk mbishi  ni uwezo wa nikk mbishi ni kustick ndani ya maada aliyo pewa na DJ FETTY na kufanya bonge moja la freestyle. Na kuweza kutoa  mitindo huru malidadi na bora. Mitindo huru aliyo wahi kuifanya nikk mbihsi hapa bongo ni mingi but  kwa muda mrefu naweza sema hii ni moja kati ya "ONE OF THE BEST OF NIKK MBISHI OF ALL TIME, Pata kuisikiliza freestly hiyo hapo juu utakubaliana na mimi.


FID Q ANENA KUHUSU "WALK IT OFF" OFFICIAL VIDEO.


  

Fid Q a.k.a King of hip hop in TZ akili kuwa "Walk It Off" ni moja Kati ya video zake bora alizo kwisha fanya Kati Miaka 16 ya mziki wake wa hip hop TANZANIA.

Pia Fid Q amekili kuwa hii ni moja kati ya video iliyo weza kumuongezea Idadi kubwa sana ya mashabiki Africa na nje ya africa kiujumla. 

Video hii hapa itazame 







NASH MC NI SAUTI YA MTAA.



NASH MC ni moja kati ya  rapper wanao unda kundi la milaba minne(wachache wanalijua hii) linalo patikana katika kundi mama la TAMADUNI MUZIK ndani ya label kongwe "MUSIC LABORATORY" nash ni moja kati ya rapper wenye misimamo mikali ya mziki, pia nash anatambulika kwa uwezo wake wa uandishi wa mashairi na utumizi fasaha wa  lugha ya kiswahili katika mziki wake

Nash Mc anata umaarufu mkubwa kwenye mziki wa hip hop TANZANIA kwa uwezo wake wakusimamia movement kubwa na zenye changamoto kubwa peke yake na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na mitaa hudhililisha mapenzi yake kwa ku support movement zake na mziki wake kiujumla 


Hili limeonekana hivi karibu pale mashabiki zake walivyo amua kudhihilisha hili mitaa kwa ku print jina la rapper huyo kwenye walls za mitaa na kuonesha kuwa wana mpenda sana nash na wanakubali anachokifanya 

MKESHA WA PASAKA KINA HAPPEN.



Mkesha wa pasaka kina happen pale msasani club, hapa SONGA a.k.a "Samaki mwenye kiu ndani ya maji" pale ONE INCREDIBLE a.k.a "moko wa miujiza" kati NIKK MBISHI, kuna nini tena zaiidi ya burudani na fulaha kwa pamoja, njoo wewe na wanao kwapamoja tu sherehekee  mkesha wa pasaka kihiphop zaidi

kiingilio ni Tsh. 7000/= kwa mtu mmoja na Tsh. 10000/= kwa watu wawili ni bei fair kabisa kwa mtanzania wa kawaida anaweza kuikidhi lengo kuu ni kutoa burudani kwa watu wenye uwezo wa chini na juu kwa pamoja. (Amka Mtanzaia) muda ndio huu.

NEW AUDIO: NIKK MBISHI - HIP HOP HOORAY MP3.


                           
Nikk Mbishi

Hapa pakua new track toka kwa nikk mbishi Hapa Mwimbo unakwenda kwa jina la HIP HOP HOORAY.

Ni moja kati ya nyimbo kali toka kwa nikk, kwani siku zote linapo kuja swala la utunzi wa mashairi bora na yenye ujumbe katika jamii nikk huwa hafanyi kosa hata siku moja.

NEW VIDEO: GOD ZILLA - I GET HIGH




Bonge la ngoma plus video kali na yenye high quality, nilichopenda zaiidi kwenye hii video ni flow za jamaa na mashairi mazuri vinanifanya kuzidi kumuamini kuwa ni moja kati ya Emcee bora Tanzania. Video itazame hapa God Zilla - I get High 


Unawaze itazama hapa chini na kutoa mawazo yako kuhusu video hii.. ?





NEW AUDIO: ZAIID - KIMBAUMBAU




                   

Download new music toka kwa zaiid kimbaumbau, kama kawaida yake mchaff hafanyi kosa kwenye flow na midondoko. Zaiid - Kimbaumbau Mp3

TIME YA KULETA USHINDI WA HIP-HOP NYUMBANI

                       
                       

Tuma neno "Kora 123" kwenda +248984000 kumpigia kura wakazi katika tuzo za kora kama "Best Hip Hop Act" wakazi anahitaji support kubwa sana kutoka kwetu watanzania kwani kumsupport kwetu wakazi ni kuleta ushindi nyumbani na fulaha kwetu watatanzania kiujumla. Hivyo basi kwa muda wako na nafasi yako please mpigie kura kwa kutuma "Kora 123" kwenda +248984000 tulete ushindi nyumbani.