TRACK OF THE WEEK - NIKK MBISHI ft NURUEL - AU


                             


Pakua Free "Track Of the Week" Nikk Mbishi ft nuruel - Au Mp3, Tangu nisikikilize track zote za nikk mishi sijawahi sikia track ya mapenzi kali kama hii kuanzia mpangilio wa matukio na visa. Kwenye kiitikio kama ilivyo kawaida yake nuruel hajafanya makosa pakua hapa Click Here Na usikilize madini haya.

RAPPER WAKAZI ATEULIWA KUWANIA TUZO ZA KORA KATIKA KIPENGELE CHA "BEST HIP-HOP ACT"

 
tanzania rapper wakazi



Habari njema kwa mashabiki wote wa rapper wakazi, Ni kwamaba siku zote ukifanya kitu kizuri mafanikio ni lazima yatakufata haijalishi eneo ulilopo au aina ya lugha unayotumia kuwakilisha mziki wako. Kwa mara ya kwwanza kwa rapper wakazi ametauliwa kuwani katika tuzo za KORA katika kipengele cha best hip hop act kwa africa.

Rapper wakazi anachuana vikali na rapper wezake wakali kutoka afrika akiwemo rapper kama SARKODIE kutokea GHANA, STANLEY ENOW kutokea CAMEROON, HAMZAOUI MED AMINE kutokea TUNISAI, Kiff No Beat (Cote D'voire) na Rapper KO kutokea SOUTH AFRICA.

Shindano hili la KORA MUSIC AWARD litafanyikia katika mji wa Windhoek Namibia mnamo tarehe 20th 2016, Maswala ya upigaji na njia za kutumia kupiga kula mtafahamiswa . Pia rapper wakazi amefulahisha sana na kitendo hichi cha kuchaguliwa kuwa miongoni mwa marapper watakao shindanishwa katika tuzo hizo za kora music award. Wakogwe wa mziki na harakati za mziki wa hip hop kama ZAVARA na Xsamiasiku4saa4 wamempa bara zote na kumsihi kuwa ushindi wake katika tuzo hizo ni ushindi wa marapper wote wa bongo.

                                      
Pia ikumbukwe kuwa rapper wakazi atakuwa anachuana vikali na rapper wekaze wakali na wakubwa bara afrika, Kwa hiyo swala la kumpigia kula ni swala la muhimu sana ili kufanikisha swala hii na ushindi kwa nchi yetu na fulaha kwa mziki wa bongo pia. Upatapo taarifa hizi mjulishe na mwezako kuwa rapper wakazi anahitaji support yako.

                                        





NEW TRACK COMING SOON 7th December - JAY MOO ft DEDDY "HILI GAME"



J moo - Hili game


Kama ilivyo ada wakubwa na wadongo yule rapper mkongwe na na mahili wa uandishi wa mashairi  katika mziki wa bongo hip hop si mwingine ni "Mjukuu Wa Mchopanga" a.k.a Jay Moo anakuletee track mpya akiwa amemshirikisha deddy,  Kama ni mfatiliaji wa mziki wa bongo hip hop kwa muda mrefu huwezi kubishana na mimi kuwa Jay moo ni moja kati ya rapper siku zote wanaounda list ya rapper bora kumi wa mziki wa hip hop kwa hapa kwetu bongo. Siku zote Jay moo anapoamua kufanya kitu huwa hakosei. Uwezo wa Jay moo kiuandishi ni mkubwa sana kitu kinachofanya watu wengi kuendeleea kumpenda hata kama hana tracks mpya hewani.

Tarehe 7 ya mwezi wa kumi na mbili kaa tayari kwa mziki mzuri na makini kutoka kwa watu makini. Track hii mpya ya Jay moo imefanyika katika studio za BONGO RECORD chini ya usimamizi wa producer P-Fank Majani, Hii nayo ni habari nzuri kwa sisi wafatiliaji wa mziki wa hip hop Jay moo anapo kutana na producer wake wa siku nyingi siku zote hakihalibiki kitu.  Kaa tayari shabiki kwa mziki wa wateule mziki ulioenda shule...........!!!.



HAPPY BIRTHDAY- FREDRICK BUNDALA a.k.a SKY WALKER




Hakika ukitaja kati ya watangazaji walio wahi kukonga nyoyo za wasikilizaji wengi wa redio hususa katika maswala ya kimziki hususa bongo fleva na hip hop Tanzania huwezi kuacha kumtaja Fredrick Bundala a.k.a Sky Walker. Sky kama ilivyo kawaida ya wadau wengi wa mziki hupendelea kumuita siku zote kwa kutumia jina hilo amekuwa mstari wa mbele kutoa mchango wake wa hali na mali kuendeleza na kusupport mziki wa kitanzani toka akiwa kama mtangazaji wa redio katika vipindi mbali mbali vya mziki na kijamii.

Umaarufu wa sky ulianzia tokea akiwa katika redio free africa katika kipindi kama "Extra Show Time" uwezo wake mkubwa wa kuweza kufahamu mziki wa kibongo hata wa kimataifa ulimfanya kuweza kupata urafiki na wasanii wengi wa kubwa hapa ndani na nje ya nchi na kuweza kupata mashavu mbali mbali ya kutengeneza matangazo mbali mbali ya vipindi vya redio.

Kwa sasa sky alipumzika katika mambo ya utangazaji na kuhamia katika mambo ya kimitandao kuweza kupush huu mziki wa kitanzania kupitia social networks mbali mbali. Kwa sasa sky ni moja kati ya wahusika wakuu wa uandishi wa makala mbali mbali katika mtandao wa www.bongo5.com akiwepo na mwezake rafiki yake kipenzi toka enzi hizo za redio free africa George Sandu a.k.a Kid bway

Sisi kama tzhiphopnew tunapenda kutoa salamu zetu za dhati na kheri ya kuzaliwa kwako bwana sky walker na family wako. Mungu awe na wewe kati maisha yako yote. Ameni.

MANSULII ft NIKK MBISHI ft BELLE 9 - Usione Ukadhani (Audio)




Track mpya iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu kubwa sana  kutoka kwa mansuli inapatikana www.mkito.com kwa sasa. Kama unavyojua wanapokutana mansuli na nikk mbishi katika midondoko na minzani siku zote ni wakogwe wa haya mambo hawakoseagi huku belle 9 mkali wa miondoko ya kuimba akibariki kiitikio cha track hiyo ni matumaini yangu kuwa siku zote kitu kitakacho tokea hapo ni mziki mzuri tu . Jipatie nakala yako ya audio hii na kwani kwa kufanya hivyo utakuwa ume support mziki wa hiphop na wasanii kiujumla. Jina la wimbo ni "Usione Ukadhani"

YOUNG KILLER ft FID Q - 13 VIDEO.





Moja kati ya video bora kutoka kwa Young Killer kwa mwaka huu wa 2015. Ni moja ya video iliyo nifanya kuamini kuwa Young Killer ni kati ya wale rapper wanapo kutana na rapper wa kubwa na wenye uwezo zaidi yake huhakikisha hawa muuangushi rapper mkubwa na kufanya kazi kubwa inayo vutia na pevu. Kwa mwisho wa weekend hii nimeona ni share na nyie fans wa blog hii kuhusu hii video japo imetoka muda mrefu but sio vibaya kuiweka hapa tena.

HABARI NZURI KWA MASHABIKI WA JOHN MAKINI



Katika Ukurasa wa mtandao wa twitter msanii kutoka Nigeria Davido Amedhibitisha kufanya kazi na rap john makini. Muda wowote mashabiki wa Davido na john wawe makini na wajitayarishe kupata mziki mzuri sana kutoka kwa sanaii hao wawili. Nyota kwa sasa inazidi kuwa njema kwa john makini baada ya kufanya kazi na rap AKA wa Africa ya kusini na KEO sasa ni Davido. Hongera san John makini.

HAPPY BIRTHDAY FID Q.



Nachukua nafasi hii kuweza kutoa salamu zangu za dhati kumtakia heli ya kuzaliwa moja kati ya wachanaji wakali wa  mziki wa hip hop hapa Tanzania bwana fid Q. Mungu akulinde na kukutangulia katika kazi za zako zote za mikono kumbuka kuwa na sisi bado ni mashabikiki zako wa mziki wa hip hop tuna kubali kinoma na ku support kazi zako endelee kusogeza hili gurudumu la mziki wetu mbele HAPPY BIRTHDAY  TO YOUUUUUUUU NGOSHA aka MWANAMALUNDI!!!!!!!

NEW ALBUM TOKA KWA NIKK MBISHI - "UFUNUO WA UNJU BIN UNUQ"



Kama kawaida ya nikk mbishi kila siku huja tofauti na kuamini katika mziki wa hip hop unahitaji zaidi ya show na lifestyle za wasanii wa hip hop kwahiyo mashabiki wana hitaji kupewa dawa ya kuweza kutibu kiu yao ya muda mrefu hivyo nikk mbishi huandaa track zake kali kwa wingi na ni moja ya rap wenye track nyingi online zenye mahadhi ya hip hop.
Katika ya mwaka huu Nikk mbishi anajalibu kutoa moja kati ya hot album. Album hii ni moja ya album nilizo weza zisikiliza na kuzielewa UFUNUO WA UNJU BIN UNUQ ni moja ya album kali sana akiwa ameshilikiana na wasanii mbali mbali waki wemo wa tamaduni musik
Album hii inapatikana online katika tovuti ya www.mkito.com na unaweza kupitia katika ukursa wa INSTAGRAM wa nikk mbishi na kupata maelekezo jinsi ya kupata nakala yako
Fanya hivyo kuweza kusupport mziki wa hip hop Tz.

FID Q KUVUKA MIPAKA MPAKA NIGERIA KWA MKALI 2 FACE.



Ni fulaha kubwa sana kwangu kuona mziki wa hip hop Tanzania ukikua kila siku kutoka step moja kwenda step nyingine hivyo inatupa faraja hasa sisi wa dau wa huu mziki wa hip hop kuto kukata tamaa na kuamini ipo siku tutafika tunapo taka kwenda.
Swala la fulaha kimetokea baada ya mkali wa hip hop tanzania fid q kutoa tetesi katika chombo fulani cha redio kuwa mashabiki wake wakae mkao wa kula any time anaweza fanya kazi na mkali wa miondoko ya RnB 2FACE kutoka Nigeria kwani wamesha wahi kukutana nakupanga mipango hiyo since long time sema harakati zikawa zinawabana  but kwa neema za Mungu zaidi ni pale majuzi juzi  rapper fidq alipo kutana na msanii huyo alipo kuwa katika harakati za coke studio na kupanga mipango endelevu ya pale walipo ishia 
Sisi kama wa dau wa mziki tuna waombea uzima ili watupe mziki mzuri kama tunavyo talajia.

TOKA KWA ONE INCREDIBLE : NEW MIXTAPE "IDENTITY" COMING SOON.



Rapper One the Incredible ambaye ni moja Kati ya rapper wanao unda kundi la tamaduni muzik ameliweka swala hilo wazi katika ukurasa wake wa INSTAGRAM akiwataarifu wapenzi wake wa kanda mseto (mixtape) wakae mkao wakula kwani mixtape yake kali inayo kuja ambayo ipo katika hatua za mwisho wisho kabisa katika maandalizi ya kutoka.

Ni imani yangu hii itakuwa ni mixtape kali wahi tokea kwa mwaka huu wa 2015 kwani kila mtu anajua uwezo wa rapper one linapokuja swala la kunata na midundo na umahili wa uandishi..
Pia rapper One incredible amesema kwamba mixtape yake ataitoa bure kabisa bila malipo yoyote kitu ambacho ni moja kati ya vitu vilivyo fanya watu wengi waweze kutoamini swala hilo kwani itakuwa ni mala ya kwanza kutokea katika music industry ya bongo. But all in All tukae tayari kwa ajira ya "IDENTITY"

NI TIME YA RAPPER MABESTE: NDOA




Rapper mabeste yuko mbioni muda wowote kufunga ndoa na mpenzi wake mpendwa walio pendana kwa muda mrefu katika kipindi cha laha na matatizo. Rapper mabeste amelionesha hilo wazi kwa wapenzi wake kuwa anampenda sana mpenzi wake kwani hata mwanzo kipindi ana pata matatizo mabeste alikuwa bega kwa bega na mpenzi wake .Pia alipo pata tatizo kubwa  hakuona hatari kuomba msaada kwa fans wake hata wasanii wenzake. Mabeste ni rapper amabaye amefanikiwa kupata mtoto mmoja mpaka sasa.

Mabeste amefika uamzi huo baaada ya kuona  now ni muda wa yeye kuvuta jiko japo ametahadhalisha kuwa swala hilo linaweza kuwa la kushitukiza, kwahiyo watu wawe tayari kwa lolote iwe kimchngo au any support.

NEW TRACK COMING SOON P THE NATIVE ft JORDAN- CHINI YA JUA.



Kama hujawahi pata nafasi na kumsikiliza vizuri P the Native utakuwa unakosa kitu ili kukamilisha chat yako ya  underground rapper wakali katika music industry ya Tanzania. Naamini ukipata muda ukatulia na kisikia japo ngoma moja yake aliyo toa,napendekeza utafute ngoma yake inayo kwenda kwa jina la UWEZO amemshirikisha Mulla asee ni moja ya ngoma kali sana kusema  ukweli.Kinachonifulahisha kumsikiliza p tha native ni uwezo wa kutumia street language au kwa kiswahili tunaiita "lugha ya mtaa" kufikisha ujumbe kwa hadhila. Katika swala la uandishi wa beti zake itakuchukua muda kidogo kuweza kumuelewa kwani ni moja ya rapper wasio tumia mtiriliko wa uandishi uliozoeleka kitu kinacho fanya rapper wengi kutumia aina hii ya uandishi linapokuja swala la DISS.

New Joint inayokuja toka kwa P the native ni Ngoma inayokwenda kwa jina la "CHINI YA JUA" naamini ni bonge la ngoma maana always rapper bora ni bora siku zote hata kama asipotoa ngoma mpya.Mitaa ikae mkao wa kula kupokea mziki mzuri.

FID Q AINGIZWA KWENYE ORODHA YA WASANII 20 BORA WA HIP HOP AFRICA



Fid Q ni moja wa rapper bora sana walio wahi tokea katika ramani ya mziki wa hip hop hapa kwetu Tanzania,Kama kweli wewe ni mfatiliaji mzuri wa mziki wa hip hop huwezi kubishana na mimi, Kwani mpaka sasa naweza sema ni mfalme wa Hip hop Tanzania,kinacho mtofautisha Fid Q na rappers/wachanaji wengine hapa nchini ni uwezo wake wa  ki uandishi wa mashairi,linapo kuja swala la kuandika mashairi siku zote Fid Q huwa hakosei katika kuandika mashairi makali na magumu kudadavua na  pia  hutumia pia ufundi wake aliopewa na mwenyezi mungu wa kutumia lugha ya kiswahili vizuri na kuhakikisha  masharii yake yanakuwa katika kiwango chake cha juu.

Kutokana na hayo basi jalida la SA HIP-HOP limempa nafasi nyingine Fid Q kutambulika Kia afrika kwa kuweza kuamini uwezo wake wa uandishia wa Mashairi na kumuingiza katika orodha ya Majina  20 ya wasanii bora Afrika na fid Q akikamata nafasi ya 18 akiwa Mtazania pekee kupata nafasi hiyo. wasanii wengine walio unda Orodha hiyo ni kama ifuatavyo.



1. AKA - South Africa.

2.Sarkordie - Ghana.

3.Ice prince - Nigeria

4.Cassper Nyovest - South Africa

5.M.I - Nigeria.

6.KO - South Africa

7.Manifest - Ghana

8.k'naan - Somalia

9. Zues - Botswana

10. Phyon - Nigeria.

11. Olamide -  Nigeria

12. Dee Money - Ghana

13. Octopizzo - Kenya

14. Tumi - South Africa

15. Stunner - Zimbambwe

16. Yossoupha - Congo

17. Dama Da Bling - Msumbiji

18. Fid Q - Tanzania

19. Cleo ice Queen - Zambia

20. Cal Vin - Zimbambwe



Hapo ndipo Fid Q aliweza kuwa katika list hiyo na kuwa rapper bora na pekee kwa Tanzania kutokea katika jalida hilo la SA HIP-HOP.





MJUE THE BIG BOSS KUTOKA LABEL YA TAMADUNI MUZIK


Ni Time Ya Big Boss Kwenye GAME, Ni Moja Ya rapper Wanaofanya kazi Pamoja Na timu Ya Tamanduni Muzik Na Ni Mzuri sana Ki uandishi Ukipata Time Hebu Msikilize vizuri.

KAA TAYARI KWA NGOMA KALI: P THE EMCEE ft YOUNG KILLER ft DULLY SYKES.



Jana ilikuwa siku Njema Kwa P the emcee na Young killer plus Mkongwe wa Bongo Fleva Dully kukutana Studio kutegeneza Bonge la ngoma kama P anavyo bainisha kwenye ukurasa wake wa Instagram
Ngoma Hiyo inayokwenda kwa Njina La RUN DSM ikokaribu kutoka Out.
Naamini itakuwa ngoma kali sana maana P THE EMCEE Na Young Killer ni Moja Ya rappers wa kali sana kiuandishi na unataji na midundo. Dully always huwa hatuangushi fans wake,TUWE TAYARI KWA MIKONO MIWILI KUIPOKEA NGOMA.

NEW ALBUM: GETTO AMBASSADOR - UWANJA WA FALISAFA.



Pata New Album inayokwenda kwa jina la UWANJA WA SALISAFA toka Kwa rapper Getto Ambassador a.k.a Balozi wa Getto.....

Kama Unavyojua linapokuja swala la Kunata Na Kuitumia Fasihii ipasavyo Getto Hafanyangi Kosaa Always Ana Nata Na Mdundo Na Utamshii wa Maneno na flow yake siku zote vinanipa ladha halisi Ya Kiswahili. Getto ni moja kati ya rapper wanao unda kundi la Tamanduni Muzik wengi wakimuita kama pacha wa Songa kwa sababu ya album Yao ya kwanza walifanya pamoja na walikuwa wana aina kama moja ya utumiaji wa Maneno ya kiswahili vizuri.

Pata NAKALA yako Halisi. Na hutojutia Fedha yako Kamwe nakuhakikishia Hiyoo.... Kwa mawasiliano Unaweza wasiliana naye kwa namba hizi
»» 0658528787
»» 0765272734

NEW: LIST YA KILI MUSIC AWARDS OUT..

Baadhi Ya Vipengelene Vivyomo kwenye List Hiyo Ya KILIMANJARO MUSIC AWARDS ni kama ifuatavyo....

 Wanaowania tuzo ya msanii bora wa hiphop: Joh Makini, Fid Q, MwanaFA, Roma Mkatoliki na Profesa Jay."

Wimbo bora wa Hiphop: Bongo hiphop - Fid Q , Mfalme MwanaFA , Kipi sijasikia Prof Jay, Gere - Weusi, I see me Joh, XO - Joh.

Mtunzi bora wa mwaka Hiphop: FidQ JohMakini, MwanaFA,Nikk wapili na Kala Jeremih"

 Producer bora wa bongofleva: Nahreel Man Water, Mesen Selekta, Tudd Thomas na Marcochali"

Video bora ya muziki ya mwaka: Mdogo mdogo na Nitampata wapi - Diamond, Mwana - Ali Kiba, Olethemba ya Linah, na Asante ya Ay.

Kikundi bora cha mwaka BongoFleva: Navy Kenzo, Yamoto Band, WEUSI, Makomando na B.O.B"

Mtunzi bora wa bongofleva: Ali Kiba, Diamond, Ben Pol, Barnaba na Jux.

 Wimbo bora wa mwaka: Nani kama mama C.Bella na OmmyD, Mwana -Ali Kiba, Gere - Weusi, Nitasubiri - Jux, Bongo hiphop ya FidQ"

 Wimbo bora wa Afrika Mashariki: Sura yako wa SautiSol Kioo - Jaguar, Walewale JChameleone Prokoto & Show VICTORIA_KIMANI

Hivyo Ni Baadhi Ya Vipengelene Tu katika KILIMANJARO MUSIC AWARDS unaweza fatilia Full List Katika Official Website Ya KTMA.

TEKNOLOGY MIXTAPE MTAANI

New mixtape iitwayo teknolology ya Producer wa Tamaduni Muzik aitwae REY-TEK Inapatikana Mtaani Kwa sasa.Mixtape hiyo ina Jumla Ya nyimbo 11 tofautitofauti katika mahadhi ya hiphop.Pia Ameweza kuwashirikisha wasanii mbalimbali wa tamaduni na nje ya tamaduni .Jipatie nakalaa yako Mapema Support mziki wa hiphop Tanzania Pia.

NEW TRACK: JANB-HUSTLE EVERYDAY

https://mkito.com/mobile/song/hustle-everyday/13433/

NEW TRACK: SONGA ft JEFF LEGEND

https://mkito.com/mobile/artist-profile/songa/675

NI ZAMU YA STEREO na CHIDI BENZ

Ni zamu ya Stereo na Chid Benz kwenye Game la hip hop.Ni kwa muda mrefu chid Benz na stereo wamekuwa kinywa kwenye Game bila kutoa ngoma mpya hewa. Usemi huo umevujika juzi stereo alipo achia ngoma mpya iitwayo UKONGA ILALA ni mziki wa Tofauti unaozungumzia sana mziki wa mtaani kama unavyojua stereo ni king wa mziki wa Mtaani. Kiukweli stereo na Chid Benz wameutendea haki huu Wimbo kwasababu wamezungumzia Mambo mengi.

Pata Nafasi kuutafuta wimbo huu na Kuusikia kiundani na Utaelewa nini ninacho maanisha.

MJUE MTANGAZAJI ANAYE IWAKILISHA VIZURI HIP HOP TANZANIA

Kama ulikuwa hujui Ndio Ujue kuanzia Leo,JABIR SALEH Mtangazaji Wa kituo cha redio cha Times FM ni Kati Ya Ma presenter Bora Kabisa Kuwahi Tokea Tanzania Kwa Kuwapa Support Wasanii Wa changa Na Wakubwa hasa wa Tasnia Ya Mziki wa Hiphop Nchini.
   Ame kuwa akiwaalika wasanii wengi Kwenda studio kutambulisha Kazi zao na plan zao za mziki bila shida.Pia ni Kati ya watangazaji Mwanao jua mziki wa hip hop vizuri....

Hivi Karibuni JABIR SALEH amekuwa miongoni wa Watangazaji wanao wania TUZO ya watangazaji bora Wa redio na kwa dalili zinazo endelea Mtandaoni Anauwezekano Mkubwa wa kishinda category kalibia zote alizo ingia kwa sababu watu wanaelewa anachokifanya. HUYO NDIO JABIR SALEH fatilia kipindi chake cha The jumpoff umuelewe zaidi.

TAMANDUN MUZIK WATOA CHAPISHO LA KOFIA KWA MALA YA KWANZA

Kikundi Cha Mziki Wa Hip Hop Tamanduni Muzik Cha Toa Chapisho La Kofia zenye Lebo Ya Nembo Yao Kwa Mara Ya Kwanza..... Ikumbukwe hii sio Mara Ya Kwanza Kikundi Hichi Kuanzisha Biashara Za Matangazo Ya Bidhaa Zenye Nembo Yao Kwa Mara Ya Kwanza Na Pia Wasani Wanao Patikana Katika Kikundi Hicho Wamekuwa Waki Chapisha T-shirt zenye Nembo mbalimbali Zikiwemo za Album,mixtape, hata Makongamano Yao...

  Kama Kweli Wewe Ni Mpenzi Wa Kikundi Hichi Naamini Utawaunga Mkono Kwa Vyovyote Vile Bei Ya Kofia Moja Ni Tsh.20000/= za Kitanzania
#MovementForChange Support Wasanii Wetu......

New Mixtape Mtaani [ MWENGE-KIWALANI ]

Mixtape iliyo kuwa ikisubiliwa kwa hamu kubwa mtaani sasa inapatikana kwa sasa mtaani ikiwa katika hard copy pia na online.Kiukweli hii ni mixtape ambayo rapper wengi wameikubali na kuipa go ahead mtaani kwani imekamilika na imekuwa ni mixtape ya kwanza Tanzania kukubaliwa kama mixtape bora duniani na rapper nikk mbishi
  Upatikanaji wa Mixtape hii unaweza kumfollow rapper zaiid instagram na kuidownload katika bio yake au kufanya nao mawasiliano.Fnaya haraka mixtape hii sio ya kuikosa mtu wangu.

Rapper Mwenye Uandishi Adimu Tanzania

Kama Ukitaka Kufahamu Utofauti Na Umalidadi Wa Uandishi Wa Mashairi Yaliyo Katika Mtiririko Mzuri Bila Kuhama Katika Maada Lengwa Jitahidi Kufatilia Kazi Za Rapper Huyu Anaitwa P THE MCEE ni Rapper Kati Ya Marapper Wanao Unda Kundi La TAMADUNI MUZIK. Kiuhalidhia Kabisa Jamaa Anaandika Vitu Ambavyo Ni Common Katika Jamii Japo Hajapata Airtime Ya Kutosha Katika Media Za Tanzania Lakini Ni Moja Kati Ya Rapper Wenye Uwezo Mkubwa Wa Uandishi Wa Mashairi Bora Kabisa.

Mwana FA Aachia KIBOKO YANGU official Video

Rapper Huyo Kutoka Tanga Akimshirikisha Ali Kiba King Wa Chorus Tz. Video imekuwa Kama Maana FA Alivyo Waambia Na Kuwaahidi Mashabiki Zake Kuwa Wakae Mkao Wa Kupata Video Ambayo Anaamini Kwamba Ni Bora Kuliko Video Zake Zote.
Unaweza Kuitizama Video Yake YouTube Na Kutoa Maano Yako.

Nikki Mbishi Aamua Kuacha Mziki.

Swala Hilo Mpaka Sasa Limekuwa Katika Social Media Likichukua Headlines Kubwa Sana Pale Ambapo Nikki Alitoa Tamko Hilo rasmi katika ukurasa wake wa Twitter Na Kuacha Mashabiki Wengi Midomo Wazi,Swala Hilo Linaonekana Kama Kuja Kwa Ghafula Sana,Kiasi Kwamba Hata Rafiki Zake Wa Karibu Wa Tamaduni Muzik Akiwemo Songa Alipatwa Na Mshituko,Japo Kuwa Mpata Sasa Hivi Nikki Mbishi Amesimamia Msimamo Wake.Japo kushauriwa Na Wasanii Wengi Wakiwemo Wa kongwe kama Prof J,Did Q,God Zilla.
Mpaka Sasa Mashabiki Wengi Hawaamini Swala Hilo,ila wana Amini Nikk Atabaki Akifanya Maswala Mengine Ya Kimziki Wa Hip Hop Na Sio Kuimba Tena Kama ilivyo Zoeleka.