Wakazi mpaka sasa ajatamka siku rasimi ambayo ataachia kanda mseto yake hiyo mpya kwa sababu anasema kuwa kuna baadhi ya mambo bado anayaweka sana na kama yakikaa sawa kama anavyotaka atakuwa hana kipingamizi tena cha kumfanya asiachie kanda mseto hiyo inayo subiliwa kwa shauku kubwa mtaani
Pia kuna uwezekano kuwa wakazi akawa katika mpango pia wa kuachia album yake mpya baada ya kuachia mixtape yake mpya inayo subiliwa na watu wengi mtaani na mimi nikiwa mmoja kati yao. Kama alivyo tamka katika mahojiano ya kipindi cha Ladha3600 kinacho lushwa na redio ya E-fm chini ya utangazaji wa Jabir Saleh , namnukuu;
Nitaachia Mixtape siku za karibuni kabla ya Album kwasababu kuna vitu bado havijakaa sawaHivyo mpaka sasa hatujajua tarehe na siku rasimi ambayo wakazi atatoa mixtape yake ikifatiwa na album yake mpya. Lakini kaa tayari kwa ujio wa kishindo kutoka kwa wakazi. Kinachotakuwa kwako kama shabiki wa kweli ni support yako ya nguvu ili kuweza kufikisha mziki huu wa bongo hip hop mbali zaidi ya hapa ulipo . Pia taarifa hizo utaendelea kuzipata hapa bure kwenye tovuti hii yetu pendwa.
Chapisha Maoni