NEW TRACK COMING SOON 7th December - JAY MOO ft DEDDY "HILI GAME"



J moo - Hili game


Kama ilivyo ada wakubwa na wadongo yule rapper mkongwe na na mahili wa uandishi wa mashairi  katika mziki wa bongo hip hop si mwingine ni "Mjukuu Wa Mchopanga" a.k.a Jay Moo anakuletee track mpya akiwa amemshirikisha deddy,  Kama ni mfatiliaji wa mziki wa bongo hip hop kwa muda mrefu huwezi kubishana na mimi kuwa Jay moo ni moja kati ya rapper siku zote wanaounda list ya rapper bora kumi wa mziki wa hip hop kwa hapa kwetu bongo. Siku zote Jay moo anapoamua kufanya kitu huwa hakosei. Uwezo wa Jay moo kiuandishi ni mkubwa sana kitu kinachofanya watu wengi kuendeleea kumpenda hata kama hana tracks mpya hewani.

Tarehe 7 ya mwezi wa kumi na mbili kaa tayari kwa mziki mzuri na makini kutoka kwa watu makini. Track hii mpya ya Jay moo imefanyika katika studio za BONGO RECORD chini ya usimamizi wa producer P-Fank Majani, Hii nayo ni habari nzuri kwa sisi wafatiliaji wa mziki wa hip hop Jay moo anapo kutana na producer wake wa siku nyingi siku zote hakihalibiki kitu.  Kaa tayari shabiki kwa mziki wa wateule mziki ulioenda shule...........!!!.



Chapisha Maoni